Kocha mkuu wa Yanga Hans van de Pluijm, amekili kuihofia timu ya Gor

NA MWANDISHI WETU
pluijm+photo
Kocha mkuu wa Yanga Hans van de Pluijm, amekili kuihofia timu ya Gor Mahia kutoka Kenya ambayo watakutananayo katika mchezo wa ufunguzi kwenye kombe la Kagame julai 17, Jijini Dar es salaam.
Mabingwa hao wa Ligi kuu Tanzania bara watakutana na Gor Mahia katika mchezo wa kwanza wa ufunguzi, hivyo basi kutokana na ukubwa wa vilabu hivyo inaonyesha kuwa mchezo huo utakuwa kama fainali.
Akizungumza na Mtandao huu leo asubuhi katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, Pluijm alisema kuwa, anatambua viwango vya timu zote za kundi ‘A’ lakini anaiogopa zaidi timu ya Gor Mahia hali inayopelekea kundi hilo alione gumu.
“Nafahamu timu zote zimekuja kushindana kwaajili ya kuchukua ubingwa na ninaziheshimu kwa ubora wao, ila timu ya Gor Mahia naihofia zaidi” Alisema Pluijm.
Yanga imepangwa kundi A lenye timu nne ambazo ni Gor Mahia (Kenya), Telecom (Djibout), KMKM (Zanzibar) na Khartoum (Sudan).
Wakati huo huo mshambuliaji wa Yanga Malimu Busungu, amewaahidi mashabiki wa timu hiyo wakae tayari kuona vitu vizuri kwakuwa amejipanga kuonyesha uwezo wake katika michuano ya Kagame.
Mshambuliaji huyo aliyesajiliwa na Yanga akitokea JKT Mgambo ya Tanga, ameonekana kuwa kivutio kwa mashabiki wengi waliojitokeza katika uwanja wa Karume jana na kufanya mashabiki wawe na hamu ya kuona vitu vyake akiwa uwanjani.
“Nawaahidi mashabiki wa Yanga sitowaangusha kwa kuwa nimejipanga vyema kukabiliana na mikikimikiki ya Kagame” Alisema Busungu.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *