A. SPORTS KUMALIZA NA COASTAL, KISHA KUISUBIRI SIMBA S.C

NA MWANDISHI WETU, Tanga

AFRICAN SPORTS

Kikosi cha Timu ya African Sport

BENCHI la ufundi timu ya soka African Sports ya Tanga, limesema mchezo wao wa kirafiki dhidi ya Coastal Union ya jijini humo Septemba 5, ndio utakuwa mchezo wao wa mwisho kabla ya kuwasubili Simba kwenye mchezo wao wa ufunguzi Septemba 12.

Mchezo huo wa kihistoria kwa timu hizo za Tanga, utachezwa Uwanja wa Mkwakwani, jijini humo.

Akizungumza leo na Simba Makini jijini humo kocha msaidizi wa kikosi hicho Ally Manyani alisema, wakimaliza mchezo huo wataanza kambi rasmi ya kujiandaa dhidi ya Simba.

Alisema kikosi chao hivi sasa kinaendelea na mazoezi yake ya kawaida kwenye Uwanja wa Jiwe mkoani humo.

“Kocha mkuu Mrage Kabange, amesema mchezo wetu dhidi ya Coastal Union, ndio utafunga hesabu za kikosi chetu kwenye michezo ya kirafiki na kugeukia mawindo ya michezo ya ligi kuu.

“Tunafahamu fika siku zote unapocheza na timu kama Simba, kunakuwa na ugumu kidogo, lakini sisi kama makocha tumewaandaa vyema vijana wetu kuhakikisha wanashinda mchezo huo wa ufunguzi” alisema Manyani.

Manyani alitamba kuwa wamefanya usajili mzuri kwa ajili ya kuja kufanya vizuri kwenye michezo ya ligi kuu.

Alisema kikosi chao hakijacheza ligi kuu kwa miaka 20 sasa, hivyo nafasi waliyoipata katika kupanda daraja wataitumia vyema ili wasirudi walikotoka.

“Tuna muda sasa hatujacheza ligi kuu, ndio maana tumeweza kusajili kikosi cha wanaume wanaoweza kuipigania vyema timu yetu ilete ushindani na siyo kucheza msimu mmoja alafu tukajikuta tunarudi tulikotoka” alisema.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *