SIMBA, YANGA ZAKENUA

NA MWANDISHI WETU

YangaSimba

MABINGWA watetezi wa taji la ligi kuu soka Tanzania Bara timu ya Yanga, imeonyesha ina kila sababu ya kulitetea taji lao msimu huu baada ya leo kupata ushindi wa pili mfululizo kwa kuifunga Tanzania Prisons mabao 3-0.

Yanga ambao katika mchezo wa kwanza waliwafunga Coastal Union, walikuwa mbogo muda mwingi kwenye lango wa wapinzani muda mwingi wa mchezo huo.

Wafungaji wa Yanga katika mchezo huo walikuwa ni Mbuyu Twite aliyefunga dakika ya 27 na Amis Tambwe dakika ya 45, mabao hayo yakipatikana kwa mipira ya kutenga iliyopigwa na Haruna Niyonzima ‘Fabregas’, lakini kipa wa Tanzania Prisons, Mohamed Yussuph aliitema na wachezaji hao kuimalizia.

Tanzania Prisons waliocheza soka la taratibu kwenye kipindi hicho cha kwanza washindwa kabisa kuifikisha mipira kwenye lango la Yanga.

Shambulizi lao kubwa katika kipindi ilikuwa dakika ya 31 mshambuliaji wao Jeremiah Juma, kupiga mpira wa kutenga uliopa juu ya lango la Yanga.

Mpaka mchezo huo unakwenda mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa mabao maawili, huku wapinzani wao wakicheza soka la kujihami zaidi.

Prisons walirudi kipindi cha pili na kufanya mabadiliko kadhaa, lakini dakika ya 59 alikuwa mshambuliaji Donald Ngoma aliyeipatia Yanga bao tatu kwa mkwaju wa penati baada ya beki wa Prisons James Josephat kumkwatua Msuva eneo la hatari na mwamuzi Alex Mahagi wa Mwanza kumzawadia kadi nyekundu.

Tanzania Prisons bado waliendelea kushambuliwa na Yanga, licha ya kufanya mabadiriko ya wachezaji.

Yanga, walizidi kutengeneza mashambulizi mengi langoni mwa wapinzani wao, lakini ukosefu umakini kwa safu ya ushambuliaji ndio sababu ya kuondoka na mabao hayo.

Yanga: Ally Mustapha ‘Barthez’, Hajji Mwinyi Mgwali, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondani, Thaban Kamusoko, Msuva, Niyonzima / Geofrey Mwashiuya, Ngoma, Tambwe / Malimi Busungu na Deus Kaseke / Salum Telela.

Tanzania Prisons: Yussuph / Aron Kalambo, Salum Kimenya, Lauren Mpalile, Josephat, Nurdin Chona, Jumanne Elfadhil, Lambert Sabianka, Juma Seif ‘Kijiko’, Mohamed Mkopi / Cosmas Ader na Boniface Hau / Ally Manzi.

Katika mchezo mwingine uliochezwa Uwanja wa CCM Mkwakwani, Tanga ulimalizika kwa ‘Mnyama’ Simba kupata ushindi wa mabao 2-0.

Mabao ya Simba katika mchezo huo yaliwekwa kimiani na wachezaji wake Justice Mabjavi na Hamis Kiiza.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *