AGUERO ATUPIA YOTE CITY IKISAMBARATISHA CHELSEA WEMBLEY

Mshambuliaji Sergio Aguero ameisaidia Manchester City kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Chelsea katika mchezo wa ngao ya jamii uliofanyika uwanja wa Wembley.

Mchezo huo ni ufunguzi wa ligi kuu nchini Uingereza ambayo itaanza wikiendi ijayo.

Aguero akishangilia baada ya kufunga goli la kwanza dhidi ya Chelsea

Aguero alifunga bao la kwanza dakika ya 15 akimalizia mpira wa kinda Phil Foden huku la pili akifunga dakika ya 58 akipokea pasi kutoka kwa Bernardo Silva.

Chelsea chini ya kocha mpya Maurizio Sarri walionekana kuzidiwa na City ambapo wangeweza kupokea kipigo kikubwa zaidi ya hicho.

City itaanza ligi hiyo kwa mechi ya ugenini dhidi ya Arsenal katika uwanja wa Emirates wakati Chelsea ikianzia ugenini mbele ya Huddersfield Town siku ya Jumamosi.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *