Ajib aipeleka yanga kileleni.

Mkwaju mkali uliopigwa na Ibrahim Ajib Migomba na kumshinda golikipa wa kagera Sugar Juma Kaseja umeihakikishia klabu ya yanga ushindi wa mabao 2 kwa 1 kwenye mchezo uliomalizika jioni hii katika dimba la kaitaba mkoani kagera.

Bao la kwanza la Yanga lilifungwa na Mzambia Obrey Chirwa kufuatia pasi murua iliyopigwa na Ibrahim Ajib katika kipindi cha kwanza kabla ya Ajib kuongeza la pili. Mshambuliaji wa Kagera Sugar Jafary Kibaya aliipatia timu yake bao la kufutaia machozi kufuatia mahesabu mabovu ya golikipa kwenye mpira uliopigwa katika “box” la Yanga na kumpa mfungaji nafasi ya kupiga kichwa kilichozaa bao hilo.

kwa matokeo hayo Yanga inafikisha alama 12 baada ya michezo 6, ikiwapiku wapinzani wao wa jadi Simba wenye alama 11 wakiwa na mchezo mmoja mkononi dhidi ya Mtibwa Sugar hapo kesho.

Matokeo mengine ya michezo iliyopigwa leo hii ni kama yafuatavyo.

NDANDA FC 1 – MAJIMAJI FC 1.
RUVU SHOOTING 0- SINGIDA UNITED 0
MWADUI FC 1 – AZAM FC 1
NJOMBE MJI 0 – LIPULI 0.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *