Alichozungumza Neymar baada ya kutua PSG

JIONI ya Alhamisi hii imekuwa ya furaha kwa mashabiki wa Paris Saint-Germain (PSG) baada ya klabu hiyo tajiri ya Ufaransa kukamilisha uhamisho wa Neymar kutoka Barcelona ya Hispania.

Neymar amesaini mkataba wa miaka mitano na PSG baada ya mapema leo kuwaagiza wanasheria wake kuilipa Barcelona Euro 222 milioni kama gharama za kununua mkataba wake klabuni hapo.

Baada ya kusaini mkataba huo Neymar anayetajwa kuwa nyota mkubwa wa soka sambamba na wakali Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, alizungumza na tovuti ya klabu hiyo, hizi hapa ni baadhi ya kauli zake;

Neymar akisaini mkataba na PSG

“Nina furaha isiyo kifani kujiunga na PSG.

“Tangu nimekuja Ulaya, timu hii imekuwa ni katika zinazoonyesha ushindani mkubwa na yenye malengo. Changamoto kubwa iliyonivuta kuja kujiunga na kikosi hiki ni kuhakikisha timu inabeba makombe yote ambayo mashabiki wanayahitaji.

“Malengo ya PSG yamenivuta kuja hapa, nimecheza misimu minne Ulaya, nadhani nipo tayari kukabiliana na changamoto mpya.

“Kuanzia leo nitafanya kila niwezalo kuwasaidia wachezaji wenzangu, kuipeleka timu mbele zaidi na kuleta furaha kwa mamilioni ya mashabiki wake duniani kote.

Neymar anakuwa mchezaji ghali zaidi duniani akivunja rekodi ya kiungo wa Manchester United, Paul Pogba.

 

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *