AMUNIKE ACHUKUA MIKOBA YA MAYANGA STARS

Staa wa zamani wa timu ya taifa ya Nigeria, Emmanuel Amunike ameteuliwa kuwa kocha mpya wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ akichukua nafasi iliyoachwa na Salum Mayanga.

Tangu mwezi Januari Stars haikuwa na kocha mkuu baada ya mkataba wa Mayanga kumalizika huku Hemed Morroco akikaimu nafasi hiyo.

Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema wameingia mkataba wa miaka miwili na nyota huyo wa zamani wa Barcelona na Sporting Lisbon huku kukiwa na kipengele cha kuongeza zaidi.

“Leo nimekuja kuwatambulisha kocha mpya wa timu ya Taifa ndugu Emmanuel Amunike kwa mkataba wa miaka miwili.

“Amunike atakuwa pia msimamizi wa timu zote za taifa za vijana kuanzia miaka 15, 17 na 20 mpaka ya wakubwa,” alisema Karia.

Kwa upande wake kocha Amunike amesema anafahamu changamoto za soka la Afrika na amejipanga kutoa mchango wake mkubwa kwa ajili ya maendeleo ya soka la Tanzania.

“Nalijua vizuri soka la Tanzania na ninafahamu kuna timu nzuri, siwezi kuahidi miujiza lakini nitajitahidi kuhakikisha tunajenga umoja na ili kupata mafanikio,” alisema Amunike.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *