AUBAMEYANG KUPEWA JEZI YA HENRY ARSENAL

Taarifa zinasema kuwa Arsenal wamethibitisha nyota wao mpya Pierre-Emerick Aubameyang atavaa jezi namba 14 iliyokuwa ikivaliwa na gwiji Thierry Henry.

Washika bunduki hao wa London walishindwa kutangaza jezi atakayovaa nyota huyo wakati wakimtambulisha jana Jumatano baada ya kutoa pauni 56 milioni kwa Borussia Dortmund kupata saini ya raia huyo wa Gabon.

Taarifa hiyo inasema Arsenal walimuandalia Aubameyang jezi hiyo tangu wakiwa kwenye mazungumzo kufuatia kuachwa na Theo Walcott aliyejiunga Everton.

Henry alidumu na Arsenal miaka nane akifunga mabao 228 kitu ambacho Aubameyang kuwa na deni kubwa.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *