AVEVA na KABURU walia na kucheleweshwa kwa taarifa za Uchunguzi.

RAIS wa klabu ya Simba Evans Elieza Aveva pamoja na makamu wake Geofrey Nyange Kaburu hii leo wamerudishwa tena mahabusu baada ya mawakili wa upande wa jamhuri wakiongozwa na wakili Leonard Swai kudai kua uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili vigogo hao haujakamilika.

Kesi hiyo iliyosomwa tena leo katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu, iliwaacha Kaburu na Aveva wakiwa na nyuso za huzuni na huruma baada ya hakimu kuahirisha kesi hiyo mpaka oktoba 11 itakapotajwa tena.

Julai 3 mwaka huu viongozi hao walifikishwa mahakamani na taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa nchini “TAKUKURU” wakikabiliwa na makosa matano yakiwemo ya utakatishaji fedha na kughushi malipo ya kiasi cha dola za kimarekani laki tatu ($300,000).

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *