AZAM FC YAWATOA NANE MKOPO

NA MWANDFISHI WETU,

azam-fc

MABINGWA wapya wa Kombe la Kagame 2015, Azam FC, imepanga kuwatoa kwa mkopo nyota wake nane kwa ajili ya kupata nafasi ya kucheza kwenye vikosi vingine baada ya kukosa nafasi ya kwenye kikosi cha kocha wao Sterwart Hall.

Timu hiyo imesema imeamua kufanya hivyo ili kutengeneza ushindani kwa mchezaji aliyetolewa kwa mkopo na aliyebaki kikosini.

Akizungumza na Simba Makini, Afisa Mtendaji mkuu wa kikosi hicho, Saad Kawemba, alisema wameamua kufanya hivyo ili kikosi kizidi kuwa kizuri zaidi ya ilivyo sasa na kuwepo na ushindani ndani ya timu.

Kawemba alisema, kitendo cha mchezaji kutolewa kwa mkopo ndio njia sahihi ya kumuonyesha kocha Hall kama mchezaji anaweza na kurudishwa kikosini, kuliko kufanya mazoezi huku ukiwa huchezi mechi.

“Tumepanga kuwatoa kwa mkopo baadhi ya nyota wetu ambao wamekuwa hawapati nafsi ya kuchomoza kwenye kikosi cha kwanza mara kwa mara ili wapoate nafasi ya kuonyeshja viwango vyao huko tutakapowapeleka.

“Hakuna mchezaji anayemiliki nafasi hapa Azam FC, hivyo usishangae kuona fulani katolewa kwa mkopo na Fulani amerudishwa kikosini na kuanza kucheza kikosi cha kwanza.

“Hivyo nawataka hawa ambao wataenda kwa mkopo watumie vipaji vyao kumshawishi kocha Hall na aweze kurejea tena kikosini” alisema Kawemba.

Kawemba aliwataja nyota waliotolewa kwa mkopo na kusema Brian Majegwa wa Uganda ameenda KCCA ya nchini kwao.

 

Nyota wengine ni Ismail Gambo ‘Kussi’ na Omary Wayne (Majimaji), Bryson Raphael (Yanga) Joseph Kimwaga (Simba), huku akisema nyota wengine watawaweka hadharani hivi karibuni.

 

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *