AZAM KUJIPIMA NA TIMU HIZI…

Kikosi cha Azam FC kinatarajia kuwa na mechi mbili za kirafiki katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama kupisha michuano ya Chalenji inayo endelea nchini Kenya.

Jumamosi Disemba 9 itacheza mchezo wa kwanza na Friends Rangers saa 1 usiku katika uwanja wa Azam Complex ili kuwaweka fiti wachezaji waliobaki kabla ya kujiunga na wenzao baada ya michuano ya Chalenji kumalizika.

Msemaji wa klabu hiyo Jaffer Idd amesema baada ya mchezo huo Azam itacheza mechi ya pili Disemba 13 dhidi ya Mvuvumwa United katika uwanja huo huo ili kuweka utimamu kwa wachezaji wake.

“Tulianza mazoezi siku nne zilizopita tutakuwa na mechi mbili za kirafiki dhidi ya Friends na Mvuvumwa, kikubwa ni kuendelea kukiweka fiti kikosi chetu.

“Unajua kuna wachezaji wapo kwenye timu za taifa kule Kenya kwahiyo hawa waliobaki wanatakiwa wawe vizuri ili wenzao wakirudi wawe sawa,” alisema Jaffer.

Jaffer amesema pia wanategemea kuwa na mechi nyingine za kirafiki katika siku za usoni kabla ya kuendelea kwa mikiki mikiki ya ligi.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *