AZAM KUPIMA MASHINE ZAKE MBELE YA URA IJUMAA

Timu ya Azam FC itacheza mechi yake ya kwanza ya kirafiki dhidi ya URA tangu itue nchini Uganda kwa ajili ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi.

Azam ina siku ya tatu leo nchini Uganda ambapo inatarajia kucheza mechi nne za kirafiki kabla ya kurejea Agosti 15.

Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd ameiambia Simba Makini kuwa wachezaji wote wapo katika hali nzuri licha ya hali ya hewa kuwa ya baridi na mvua kidogo.

Azam imesafiri na wachezaji wake wote iliyosajili kwa ajili ya msimu mpya isipokuwa Yakub Mohammed ambaye anaendelea kuuguza majeraha na Enock Atta Agyei aliyopo katika majukumu ya timu ya taifa ya Ghana chini ya miaka 20.

“Kambi yetu inaendelea vizuri huku Uganda, wachezaji vwapi katika hali nzuri na Ijumaa tutacheza mechi yetu ya kwanza ya kirafiki dhidi ya URA.

“Baada ya mchezo huo tutakuwa na mechi nyingine dhidi ya KCCA Vipers ambao ndio mabingwa wa Uganda na timu nyingine ambayo tutaitangaza baadae,” alisema Jaffer.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *