AZAM KUWAKOSA WANNE DHIDI YA KAGERA

Timu ya Azam FC itawakosa wachezaji wanne kwenye mchezo wa leo dhidi ya Kagera Sugar utakaofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera.

Nahodha Himid Mao na msaidizi Agrey Morris hawakusafiri na timu kutokana na kuwa majeruhi.

Mshambuliji Waziri Junior na kiungo Abubakar Salum ‘Sure boy’ nao hawakusafiri na timu kutokana na sababu mbalimbali.

Ofisa habari wa klabu hiyo, Jaffer Idd ameiambia Simba Makini kuwa kikosi kimewasili salama mkoani Kagera jana na wapo tayari kwa mchezo huo.

Jaffer amesema mchezo utakuwa mgumu na hawatawadharau wapinzani hao ambao wanapitia kipindi kigumu kwa sasa.

“Kwenye mchezo wetu wa leo tutawakosa wachezaji wanne ambao ni Himid, Sure boy, Waziri Junior na Agrey kutokana na sababu tofauti,” alisema Jaffer.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin