AZAM: MUDATHIR ATAENDELEA KUBAKI SINGIDA UNITED

Uongozi wa Azam FC umetolea ufafanuzi suala la kiungo wao Mudathir Yahya aliye kwenye kiwango bora kwa sasa kuwa ataendelea kubaki Singida United kutokana na makubaliano baina yao.

Baada ya kiungo huyo kuonyesha kiwango bora tangu ajiunge na Singida kwa mkopo kumekuwa na uvumi kuwa Azam wanataka kumrejesha kundini katika dirisha hili la usajili.

Azam kupitia kwa msemaji wake Jaffer Idd amesema kiungo huyo ataendelea kubaki na Singida mpaka kumalizika kwa msimu ambapo kama kutakuwa jambo jingine ndio wataeleza.

“Mudathir ataendelea kubaki Singida taarifa kuwa tunataka kumrejesha sio za kweli, makubaliano yetu hayasemi hivyo atakuwa huko hadi mwishoni mwa msimu,” alisema Jaffer.

Kocha wa timu ya taifa ya Tanzania, Salum Mayanga amemrejesha kiungo huyo kikosini baada ya kuwa nje kwa muda mrefu ambapo katika mchezo wa kirafiki dhidi ya Benin mwezi huu alionyesha kiwango kikubwa.

Mudathir yupo katika kikosi cha timu ya Zanzibar Heroes kinachojiandaa na michuano ya Chalenji itakayofanyika nchini Kenya kuanzia Jumapili ijayo.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *