AZAM YAISHUSHA TENA YANGA VPL

Mabao 2-1 iliyopata Azam FC dhidi ya Mbao FC yametosha kuiweka nafasi ya pili na kuishusha Yanga ambayo kesho itashuka dimbani.

Mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex ulikuwa wa kasi huku timu zote zikishambuliana kwa zamu lakini umakini ulikuwa changamoto kubwa.

Azam imefikisha pointi 44 ikiizidi alama moja Yanga itakayokuwa na kibarua kesho kwenye uwanja wa Taifa dhidi ya Stand United.

Azam imekuwa ikipata ushindi mwembamba katika mechi nyingi tangu kuanza msimu ambapo kwa sasa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa ni 14.

Timu hizo zilienda mapumziko zikiwa sare ya bila kufungana licha ya kosa kosa za pande zote huku Azam ikipoteza nafasi nyingi.

Mabao yote yalifungwa kipindi cha pili ambapo Idd Kipagwile aliyetokea benchi na Bernard Arthur huku Mbao wakipata bao lao kupitia James Msuva dakika ya mwisho kabisa ya mchezo.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *