AZAM YAJIGAMBA KUTISHA ZAIDI MWAKANI

Licha ya kufika fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi klabu ya Azam FC imejigamba kutamba zaidi mwakani kutokana na kuwa na kikosi chenye mchanganyiko wa wachezaji vijana na wazoefu.

Msimu huu Azam imefanya usajili wa kawaida ikiwekeza zaidi kwa wachezaji vijana ambao wameonyesha uwezo mkubwa mpaka sasa hali ambayo uongozi unaamini itafanya vizuri zaidi.

Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd amesema kuwa wanaendelea kuandaa kikosi chao kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye michuano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kuanzia mwakani.

“Kikosi chetu kitafanya vizuri zaidi mwakani kutokana na aina ya wachezaji tulionao ambao wengi wao ni vijana na wameonyesha uwezo mkubwa.

Tutaendelea kuwaweka pamoja na matumaini yetu ni kuwa mwakani tutapigania mataji ya ndani na nje ya nchi,” alisema Jaffer.

Jumamosi Azam itacheza mchezo wa fainali ya Mapinduzi dhidi ya URA utakaofanyika kwenye uwanja wa Amani.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

2 thoughts on “AZAM YAJIGAMBA KUTISHA ZAIDI MWAKANI

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *