AZAM YASHINDWA KUISHUSHA YANGA NAFASI YA PILI

Timu ya Azam FC imeshindwa kuishusha Yanga nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi baada ya kulazimishwa sare ya bao moja na Kagera Sugar mchezo uliofanyika kwenye uwanja wa Kaitaba.

Azam ilipaswa kushinda mchezo huo ili kupanda hadi nafasi ya pili baada ya kufikisha pointi 34 sawa na Yanga lakini wanazidiwa mabao ya kufunga.

Yanga itacheza mchezo unaofuata dhidi ya Majimaji katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam na ikishinda itakuwa mbele kwa pointi tatu.

Kagera ambao walicheza vizuri leo walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 49 lililofungwa na Juma Shemvuni.

Azam walisawazisha kupitia kwa Idd Kipagwile dakika ya 53 na kuwafanya Wana lamba lamba kuondoka na pointi moja.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *