AZAM YATAKA KUMALIZA NAFASI YA PILI VPL

Azam FC imesema imekosa ubingwa msimu huu na imeweka nguvu kwa ajili ya kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi kuu ya Vodacom ili kulinda heshima.

Azam ipo nafasi ya pili kwenye msimamo ikiwa na pointi 58 ikisalia na michezo miwili dhidi ya Tanzania Prisons na Yanga.

Wana lamba lamba hao wanatakiwa kushinda mechi hizo ikiwemo ile ya Yanga ili kutimiza lengo hilo kwani mabingwa hao wazamani wakipoteza mchezo huo watashindwa kufikisha pointi 58 ambazo watakuwa nazo Azam.

Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd amesema tayari wameshakosa ubingwa hivyo watapambana kupata nafasi pili kwa ajili ya heshima licha ya kutowapeleka popote.

“Tunataka kushinda mechi mbili zilizobaki dhidi ya Prisons na Yanga ili kumaliza nafasi ya pili kwenye msimamo ili kulinda heshima kwakua tumekosa ubingwa,” alisema Jaffer.

Azam itawakaribisha Prisons siku ya Jumapili kwenye uwanja wa Azam Complex katika muendekezo wa ligi hiyo.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *