AZAM YATINGA FAINALI KAGAME, RASMI KOMBE LINABAKI TANZANIA

Mabingwa watetezi wa michuano ya Kagame, Azam FC imeingia fainali ya mashindano hayo baada ya kuifunga Gor Mahia mabao 2-0 katika mchezo uliofanyika katika uwanja wa Taifa.

Azam ilipata ubingwa huo mwaka 2015 kwa kuifunga Gor mabao 2-0 katika dimba hilo la taifa ambapo sasa wana asilimia 50 ya kulitetea taji lao.

Mchezo huo ulianza taratibu huku mpira ukichezwa zaidi katikati ya uwanja na mashambulizi yakiwa machache pande zote.

Safu ya ushambuliaji ya Azam ilionekana kukosa makali katika dakika 90 za kawaida hasa baada ya kukosekana kwa Shaban Idd Chilunda aliyesajiliwa na CD Tenerife hali ilyopelekea kwenda katika muda wa nyongeza.

Mshambuliaji Ditram Nchimbi aliifungia Azam bao la kwanza dakika ya 93 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Gor.

Baada ya bao hilo Gor waliongeza kasi kuliandama lango la Azam kurudisha bao hilo lakini idara ya ulinzi iliyokuwa chini ya Agrey Morris na Abdallah Kheri ilitimiza majukumu yake ipasavyo.

Bruce Kangwa aliifungia Azam bao la pili dakika ya 99 baada ya kuwazidi kasi walinzi wa Gor kutokea upende wa kushoto.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *