AZAM YATOA NENO KUTIMKA KWA ARTHUR

Uongozi wa Azam FC umesema umekubali barua ya mshambuliaji wao Bernard Arthur ya kuvunja mkataba kwa maslahi ya klabu na mchezaji mwenyewe.

Juzi kulitoka taarifa kuwa mshambuliaji huyo raia wa Ghana ameamua kuvunja mkataba na Azam kwakua hapewi nafasi ya kucheza kitu ambacho kinahatarisha kipaji chake.

Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd amesema mchezaji huyo amejipima na kugundua hawezi kuendana na kasi ya Azam hivyo ameamua kuvunja mkataba.

Hata hivyo Jaffer amesema mshambuliaji huyo atasubiri mpaka ligi imalizike ili taratibu zote zifuatwe na Azam impe stahiki zake anazostahili.

“Ni kweli mchezaji wetu Bernard Arthur ameamua kuondoka Azam baada ya kuona haendani na kasi yetu, uongozi umemkubalia ombi lake tunasubiri msimu umalizike tumalizane,” alisema Jaffer.

Arthur alijiunga na Azam kutoka Liberty Professional ya Ghana katika usajili wa dirisha dogo Disemba mwaka jana kwa mkataba wa miaka miwili.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *