AZAM YAZIDI KUDONDOSHA POINTI YASHINDWA KUIFIKIA YANGA

Azam FC imeendelea kudondosha pointi kufuatia kulazimishwa sare ya bila kufungana na Lipuli FC katika mchezo wa ligi kuu uliopigwa katika dimba la Samora mkoani Iringa.

Mwishoni mwa juma Azam ilibanwa mbavu na Kagera Sugar kwenye uwanja wa Kaitaba na kuwafanya kuambulia pointi mbili katika mechi mbili za mikoani.

Mabingwa hao wa kombe la Mapinduzi walizidiwa ujanja na Lipuli ambapo kama wangeweza kuzitumia vizuri nafasi walizo tengeneza wangepata pointi zote tatu.

Endapo Singida United iliyo nafasi ya nne itashinda mchezo wake dhidi ya Kagera Sugar itaishusha Azam hadi nafasi ya nne kwani itafikisha pointi 36.

Azam imefikisha pointi 35 ikiwa nafasi ya tatu baada ya kushuka dimbani mara 19.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *