AZAM:HATUSAJILI MCHEZAJI YOYOTE KUTOKA SIMBA, YANGA

Baada ya kuzagaa taarifa kwenye vyombo vya habari kuwa klabu ya Azam inataka kumsajili kiungo Papy Tshishimbi uongozi wa ‘Wana lamba lamba’ hao umesema hauwezi kusajili mchezaji kutoka timu za Simba na Yanga.

Kiungo huyo raia wa DR Congo anayechezea Yanga yupo kwenye kiwango bora kwa sasa ambapo taarifa za kutaka kujiunga na Azam zimechukua nafasi kubwa kwenye vyombo vya habari hasa magazeti na mitandao ya jamii.

Tetesi hizo zilichukua nafasi kubwa katika siku hizi kufuatia kufunguliwa kwa dirisha dogo la usajili kesho litakalodumu kwa mwezi mmoja.

Msemaji wa klabu hiyo Jaffer Idd amesema moja ya sheria ya klabu hiyo ni kutosajili mchezaji yoyote kutoka katika timu za Simba na Yanga hivyo Tshishimbi hana nafasi kwenye kikosi chao.

“Hizo ni tetesi tu, hatuna mpango wa kumsajili Tshishimbi na sijui taarifa hizi zimetoka wapi. Hatuna mpango wa kumsajili kabisa.

“Tshishimbi ni mchezaji mzuri na tunaheshimu sana kipaji chake lakini kwakua yupo Yanga amekosa sifa ya kuchezea Azam,” alisema Jaffer.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *