Baada ya Costa kuweka ngumu, Chelsea wakimbilia Torino

LONDON, Uingereza

MIAMBA ya London Chelsea ‘The Blues’ imerejesha mazungumzo juu ya kumnasa mshambuliaji wa Torino Andrea Belotti akiwa mbadala wa mshambuliaji mtukutu Diego Costa aliyeigomea klabu yake kurejea na kufanya mazoezi na kikosi cha akiba cha klabu hiyo.

Belotti amekuwa akihusishwa na klabu mbalimbali barani Ulaya ila hivi karibuni bei iliyowekwa na Torino imezikwamisha klabu nyingi na kupelekea kukata tamaa katika kinyang’anyiro hicho hali iliyoibakisha Chelsea pekee ikianzisha mchakato huo upya.

 

Dau la Paundi 90 milioni ndicho kiasi ambacho Torino wataridhia na kumuachia mshambuliaji huyo raia wa Italia huku wakisisitiza hakutakuwa na mazungumzo chini ya hapo.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *