BAADA YA AC MILAN, ARSENAL YAIPIGA WATFORD

Washika bunduki wa London, Arsenal wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Watford kwenye mchezo wa ligi kuu Uingereza.

Alhamisi iliyopita Arsenal ilipata ushindi wa mabao 2-0 mbele ya AC Milan kwenye michuano ya Europa mtanange uliopigwa uwanja wa San Siro.

Kabla ya michezo hiyo Arsenal ilikuwa imepoteza mechi nne mfululizo katika michuano yote ikiwemo fainali ya Carabao.

Peter Cech amefikisha Clean sheet ya 200 Tangu atue kwenye ligi ya uingereza
Katika mchezo huo mlinda mlango wa Arsenal, Petr Cech alifikisha michezo 200 bila kuruhusu nyavu zake kuguswa ‘Clean Sheet’.

Matokeo hayo yameifanya Arsenal kufikisha pointi 48 ikiwa nafasi ya sita alama nane nyuma ya Chelsea iliyo nafasi ya tano.

Mlinzi Shkodran Mustafi aliipatia Arsenal bao la kwanza kwa kichwa dakika ya nane baada ya kumalizia mpira wa adhabu uliopigwa na Mesut Ozil.

Pierre Emerikh Aubameyang aliifungia Arsenal bao la pili dakika ya 59 kabla ya Henrikh Mkhitaryan akimalizia la mwisho dakika ya 77.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *