BAADA YA KIPIGO KOCHA WA ITALIA AKIRI WANA KAZI KUBWA YA KWENDA URUSI MWAKANI

Meneja wa timu ya taifa ya Italia ‘Azzuri’ Giampiero Ventura amesema anahitaji wachezaji wake wawe kwenye kiwango bora katika mchezo wa pili wa mtoano dhidi ya Sweden ili isitokee wakashindwa kufuzu fainali za dunia tangu mwaka 1958.

Sweden imeshinda mchezo wa kwanza kwa bao moja jana kwenye uwanja wa Friends Arena lililofungwa na Jakob Johansson.

Sweden ilikuwa bora zaidi kipindi cha kwanza lakini Azzurri walibadilika waliporudi kipindi cha pili.

Italia itakuwa bila kiungo wao nyota Marco Verratti anayetumikia adhabu ya kadi siku ya Jumatatu kwenye uwanja wa San Siro ili kupata tiketi ya kwenda Urusi.

Ventura alisema “matokeo haya ni adhabu, matumaini yetu tukifika Milan kila kitu tutakiweka kwa ajili ya mchezo huu.

“Tunahitaji matokeo ya ushindi tu kwenye mchezo huu, tunapaswa kufanya kila linawowezekana kushinda. San Siro inapaswa kutupa ushindi lakini tunapaswa kuwa kwenye kiwango bora,” alisema Ventura.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *