BAADA YA KUTOLEWA SPORTPESA MOROCO ATAKA KUIMARISHA KIKOSI

Kocha mpya wa timu ya Singida United, Hemed Moroco amejipanga kufanya usajili mkubwa ili kuimarisha kikosi chake baada ya kutupwa nje ya michuano ya SportPesa Super Cup.

Singida imetolewa jana kwenye michuano hiyo na Gor Mahia baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 ambapo itacheza na Kakamega Homeboyz kutafuta mshindi wa tatu.

Morocco amesema wanahitaji kupata mshambuliaji wa kiwango cha juu kwa ajili ya mashindano mengine yajayo.

Kocha huyo wa zamani wa timu ya Zanzibar Heroes amesema ameona mapungufu kadhaa kwenye kikosi chake ambapo atahitaji kuongeza nguvu mpya.

“Tunahitaji kufanya usajili kuimarisha kikosi kwa ajili ya mashindano mengine yajayo kwakua kwa sasa kikosi kina mapungufu makubwa,” alisema Moroco.

Kocha huyo ameongeza kuwa anaamini atafanya vizuri katika mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu dhidi ya Kakamega siku ya Jumapili saa 7 mchana.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *