Bafana Bafana na Senegal kukata mzizi wa fitina leo.

Mchezo kati ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) dhidi ya Simba wa Teranga, Senegal utarudiwa leo hii baada ya FIFA kuamuru kufutwa kwa matokeo ya mchezo wa awali wa kuwania kufuzu kombe la dunia uliomalizika kwa ushindi wa mabao mawili kwa moja kwa wenyeji Afrika kusini, kutokana na tuhuma za upangaji wa matokeo.

Mchezo huo utafanyika nchini Afrika Kusini katika dimba la Peter Mokaba, manispaa ya Polokwane mnamo majira ya saa mbili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Afrika kusini inashika mkia katika kundi D ikiwa na alama nne wakati wapinzani wao Senegal wakiwa vinara wa kundi hilo kwa kufikisha alama nane baada ya michezo minne.Endapo Senegal itafanikiwa kushinda mchezo wa leo itajihakikishia nafasi ya kushiriki kombe la dunia nchini Urusi mwakani.

Msimamo wa kundi D.

Akizungumiza ugumu ulioukuwepo mbele yao Afrika ya Kusini, mlinzi wa Bidvest, Thulani Hlatshwayo amewatoa hofu wananchi wa taifa hilo,akiamini kikosi hicho kinaweza kushinda michezo yote miwili dhidi ya Senegal iliyosalia na kuipeleka Afrika kusini kombe la dunia.

Binafsi naamini tunaweza kuvuka dhidi ya Senegal na nikiwa kama mchezaji nafahamu umuhimu wa michezo hii kwetu. Ntakupa mfano: tulicheza na Nigeria wakiwa katika kiwango bora sana, lakini tulitulia tukacheza kwa nidhamu nakufuata mpango wa mchezo tuliopanga na tulifanikiwa kupata ushindi nyumbani kwao [Nigeria].Alisema Thulani

Senegal itaingia kiwanjani ikiwa na nyota wake wote wakiongozwa na Sadio Mane, huku Afrika kusini wakiwa na hatihati ya kumkosa mlinda mlango wao, Itumeleng Khune aliyeumia katika mchezo wa ligi kuu nchini humo mwisho wa juma hili.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *