BANKA ASAINI MIAKA MIWILI YANGA

Kiungo Mohammed Issa ‘Banka’ amesaini miaka miwili kuitumika klabu ya Yanga akitokea Mtibwa Sugar ya Morogoro.

Banka ambaye ana kasi hasa akishambulia kutokea pembeni alikuwa na msimu mzuri akiwa na Mtibwa kitu kilichozivutia klabu mbalimbali nchini kabla ya hii leo kujiunga na Yanga.

Mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu hiyo, Hussein Nyika amesema usajili bado unaendelea na amewatoa hofu wapenzi na mashabiki wa Yanga kuwa watafanya vizuri licha ya kupitia kipindi kigumu kiuchumi.

“Leo tumefanikiwa kumsajili kiungo Mohammed Issa kutoka Mtibwa kwa mkataba wa miaka miwili. Hakuna asiyejua uwezo wake na tunaamini atatusaidia sana msimu ujao,” alisema Nyika.

Kwa upande wake Banka amesema anafahamu kuwa anapaswa kugombania namba ndani ya kikosi hicho na amejipanga kufanya mazoezi makali ili kumshawishi kocha Mwinyi Zahera ampe nafasi.

“Napenda kuwaahidi Wanayanga kuwa furaha yao ya zamani itarejea ninachohitaji ni ushirikiano ili kufanikisha jambo hili,” alisema Banka.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *