Barcelona waondoa picha za Neymar Nou Camp

WAKALI wa soka la ‘kitabuni’, Barcelona wameondoa picha za Neymar kwenye kuta za uwanja wa Camp Nou ikiwa ni ishara ya kujiandaa kuendelea na maisha bila nyota huyo wa kibrazili.

Straika huyo mwenye miaka 25 ambaye anatajwa kama mchezaji nyota zaidi baada ya Messi na Ronaldo Jumatano hii amevunja ukimya wa wiki kadhaa baada ya kuwaambia wachezaji wenzake kuwa anataka kuendelea na maisha sehemu nyingine baada ya kubeba makombe manne kikosini hapo.

Thamani ya mchezaji huyo imetajwa kuwa ni Euro 222 milioni (£198 milioni) ambayo inasemekana PSG wapo tayari kulipa ili wamsajili ‘fundi’ huyo wa mpira.

Kutokana na sakata hilo kuendelea kushika kasi, wababe hao wa Katalunya hawakupoteza muda badala yake wakaanza kubandika picha za wachezaji wengine baada ya kuziondoa za Neymar kuelekea msimu mpya wa ligi unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Mashabiki wa Barcelona nao wameshindwa kuzuia hisia zao na kuamua kubandika matangazo yanayomtaja Neymar kama msaliti.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *