BELLAMY ATAKA KUMRITHI COLEMAN WALES

Nyota wa zamani wa timu ya Liverpool Craig Bellamy ameonyesha nia ya kutaka kufundisha timu ya taifa ya Wales ambayo ndio nchi aliyo zaliwa.

Baada ya kocha Chris Coleman kuachana na timu hiyo wiki iliyopita na kujiunga na Sunderland, Bellamy anaona anaweza kuchukua mikoba hiyo.

Kwa sasa Bellamy anafanya kazi katika timu ya vijana ya Cardiff, pia aliwahi kufanya kazi katika timu za vijana za taifa hilo kabla ya kuweka wazi kuwa anataka kibarua hicho.

Bellamy amecheza mechi 78 na timu ya taifa ya Wales kabla ya kutundika daruga mwaka 2013

“Naitamani hiyo kazi hata sasa hivi niko tayari, naipenda nchi Wales, nataka kuifikisha kwenye kilele cha mafanikio.

“Wachezaji wazuri wapo, kuna vijana wanafanya vizuri kwa sasa, kunatakiwa kupatikana mtu anayeweza kuwaunganisha na kazi hiyo mimi naiweza,” alisema Bellamy.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *