Belotti Aipiga Chini United, Sasa Anukia Chelsea

TURIN, Italia
CHELSEA ipo mbioni kukamilisha usajili wa mshambuliaji wa Torino Andrea Belotti baada ya kuizidi kete Manchester United ambayo ilikuwa karibu kumnyakua mshambuliaji huyo raia wa Italia.

Belotti alijiunga na Torino Agosti 14, 2015 akitokea Palermo kwa ada ya paundi 7.5 milioni ambapo sasa amekuwa lulu barani Ulaya baada ya klabu mbalimbali kuhitaji kupata saini yake.

Uwepo wa kocha wa Antonio Conte katika kikosi cha Chelsea kunafanya dili hilo kukaribia kukamilika kutokana na ukaribu wake na mchezaji huyo kwakuwa wanatokea nchi mmoja.

MAIN-FC-Torino-v-AC-Milan-Serie-A

Belotti ambaye ana mkataba wenye thamani ya paundi 84 milioni klabuni hapo huenda akaondoka na kutimkia darajani kwa bei chini ya hapo akitaka kujiunga na Chelsea badala ya Manchester United.

Sababu kuu ya mshambuliaji huyo kuibwaga United ni kutokana na klabu hiyo kutojihakikishia nafasi ya kushiriki klabu bingwa barani Ulaya.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *