BILIC: TUMEWATOA SPURS ILA KAZI BADO NGUMU

Licha ya kutokea nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Tottenham Hotspur kocha Slaven Bilic wa West Ham amekiri kuwa bado wana kazi kubwa ya kufanya.

Huu ni ushindi muhimu kwa Bilic ambaye timu yake ipo juu kwa tofauti ya mabao katika timu zilizo kwenye mstari wa kushuka daraja.

Andrew Ayew akishangilia bao lake.

“Nimefurahi kwa ushindi,hasa kwa kufuzu hatua ya robo fainali.Ila bado tuna kazi kubwa, hatujafanya kitu chochote tunapaswa kuendelea kufanya hivi,” alisema Bilic.

Raia huyo wa Serbia amesema aliwapumzisha baadhi ya wachezaji lakini mabadiliko waliyofanya yalikuwa chanya na vijana wake hawaku muangusha.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *