BILO ALIA NA WAAMUZI KIPIGO CHA JANA CHA YANGA

Kocha msaidizi wa timu ya Stand United, Athumani Bilal ‘Bilo’ amesema moja ya sababu iliyosababisha kukubali kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Yanga jana ni kutokana na waamuzi kushindwa kutafsiri vizuri sheria 17 za soka.

Kabla ya mchezo huo kocha huyo alinukuliwa akisema wataishikisha adabu Yanga kutokana na kujiandaa vizuri ingawa hali ilikuwa tofauti baada ya dakika 90.

Stand walicheza vizuri hasa kipindi cha pili kwa kuliandama lango la Yanga huku mshambuliaji wao Bigirimana Blaise akikosa nafasi za wazi ambazo zingeweza kuwapa matokeo chanya kwenye mchezo huo.

Bilo amesema waamuzi walishindwa kutafsiri vizuri sheria za soka na kuwanyima baadhi ya stahiki zao uwanjani na kupelekea kipigo hicho.

“Tumepoteza mchezo wetu, tutajipanga kwa mechi zijazo lakini sijaridhishwa na uchezeshaji wa waamuzi wa mechi kuna vitu walikuwa wanatubana,” alisema Bilo.

Stand imebaki na pointi zao 22 wakiwa nafasi ya 11 alama sita juu ya wanaoburuza mkia Njombe Mji.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *