BOCCO AMPIKU OKWI ATWAA TUZO YA LIGI JANUARI

Nahodha wa timu ya Simba John Bocco ‘Adebayor’ amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa ligi kwa mwezi Januari baada ya kumpiku nyota mwenzake Emmanuel Okwi na Awesu Awesu wa Mwadui FC.

Bocco amecheza mechi tatu mwezi Januari akifunga mabao matatu na kusaidia mengine mawili huku akicheza dakika zote 270.

Nyota huyo wa zamani wa Azam FC ametengeneza ushirikiano mkubwa na Okwi katika idara ya ushambiliaji wa Simba ambapo kwa pamoja wamefunga mabao 21.

Kutokana na ushindi huo Bocco atazawadiwa tuzo, kisimbuzi cha Azam TV na fedha taslimu sh. milioni moja kutoka kwa mdhamini mkuu wa ligi kampuni ya Vodacom Tanzania.

Bocco anatarajia kuingoza Simba jioni ya leo jioni katika mchezo wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Gendarmerie Nationale ya Djibouti utakaofanyika uwanja wa Taifa.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *