BRAZIL NAYO ‘OUT’ KOMBE LA DUNIA

Timu ya taifa ya Brazil imeungana na miamba ya soka duniani kuaga michuano ya kombe la dunia baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Ubelgiji katika mchezo wa robo fainali.

Mabingwa hao mara tano wa dunia walikuwa wakipewa matumaini makubwa ya kufanya vizuri kutokana na aina ya wachezaji iliyonayo.

Mataifa kama Ujerumani, Argentina, Hispania na Ureno yalipewa nafasi ya kufika mbali lakini ikawa tofauti na kutolewa hatua za awali.

Ubelgiji walipata bao la kwanza dakika ya 13 baada ya Fernandinho kujifunga katika jitihada za kuokoa mpira wa kona uliopigwa na Nacer Chadli.

Kelvin De Bruyne aliifungia Ubelgiji bao la pili dakika ya 31 kwa shuti kali la chini chini baada ya kupokea pasi ya Romelu Lukaku.

Renato Augusto aliipatia Brazil bao la kufuatia machozi dakika ya 76 kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Phillipe Coutinho.

Ubelgiji watacheza na Ufaransa katika nusu fainali ya michuano hiyo siku ya Jumanne.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *