BREAKING NEWS: Mbonde Atua Msimbazi Kumrithi Banda

BEKI mahiri wa Mtibwa Sugar ya mjini Morogoro, Salim Mbonde leo hii amejiunga na Wekundu wa Msimbazi, Simba kwa mkataba wa miaka miwili.

Simba imekuwa ikimfukuzia beki huyo kwa muda mrefu lakini taarifa za kuondoka kwa Abdi Banda ziliongeza kasi yao na leo wamefanikiwa kupata saini ya ‘mkoba’ huyo.

Mbonde kushoto akisaini mkataba mbele ya wakili Hussein Kitta ambaye pia ni mwenyekiti wa tawi la Simba Makini

Mbonde ametua nchini alfajiri ya leo akiwa na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kutoka Afrika Kusini ilikoshiriki michuano ya COSAFA na kufanikiwa kuibuka washindi wa tatu.

Simba inaendelea na zoezi la usajili licha ya viongozi wake wakuu kushikiliwa na vyombo vya dola huku walioteuliwa kukaimu wakiwaondoa hofu wanachama wa klabu hiyo kuwa kila kitu kitakwenda sawa.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *