CANAVARO AWATAKA MASHABIKI KUJITOKEZA KWA WINGI KESHO TAIFA

Nahodha wa timu ya Yanga, Nadir Haroub ‘Canavaro’ amewataka wapenzi na mashabiki wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi katika mchezo wao wa kesho wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda.

Mchezo huo utafanyika saa 1 moja usiku katika uwanja wa Taifa, Dar es Salaam ambapo Yanga itapaswa kushinda ili kujiweka kwenye mazingira mazuri kufuatia kupata kipigo cha mabao 4-0 kutoka USM Alger katika mchezo wa kwanza.

Canavaro amesema anafahamu kuwa washabiki wao hawajitokezi kwa wingi kutokana na timu hiyo kufanya vibaya lakini amewataka kujitokeza kwa wingi kesho kwakua ni mchezo wa kimataifa na wameweka nguvu kubwa huko.

Nahodha huyo amesema wanatarajia kupata ushindani mkubwa kutoka kwa Rayon kwakua wana timu nzuri na ina wachezaji wenye ubora lakini wamejiandaa kuhakikisha wanapata na ushindi katika uwanja wa nyumbani.

“Nichukue nafasi hii kuwataka mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi kesho, timu inahitaji mashabiki na mashabiki wanahitaji timu kwahiyo wanapaswa wajitokeze kwa wingi kuja kutusapoti.

“Mchezo utakuwa mgumu Rayon ni timu nzuri, niliwatazama kwenye mchezo dhidi ya Gor Mahia nikawaona walivyo imara lakini tumejipanga kuwadhibiti,” alisema Canavaro.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *