CECAFA YAPANGUA RATIBA YA VPL

Michuano ya ukanda wa Afrika Mashariki na Kati CECAFA, maarufu kama Challenge Cup imepangua ratiba ya ligi kuu ya Vodacom baada ya Tanzania kuthibitisha kushiriki michuano hiyo itakayofanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 25 hadi Disemba 9 mwaka huu.

Michuano hiyo itawakilisha nchi 12 za ukanda huo ambapo kwa kawaida Tanzania hutoa timu kutoka bara ‘Kilimanjaro Heroes’ na visiwani huwakilishwa na ‘Zanzibar Heroes’.

Ofisa Mtendaji mkuu wa bodi ya ligi, Boniface Wambura amesema kutakuwa na mabadiliko kidogo ya ratiba kupisha michuano hiyo ambayo ilikosekana kwa miaka miwili mfululizo.

Tutaandika barua kwa vilabu kuhusu mabadiliko haya na hii inatokana na kuwa hatukuwa na uhakika wa kufanyika kwa sababu hayakuwepo kwa miaka miwili, ratiba ya ligi yetu itakuwa na mabadiliko kidogo,” alisema Wambura.

Wambura alisema italazimika kwa timu kucheza katikati ya wiki na mwisho wa wiki ili ratiba isiwe nyuma sana kupisha michuano hiyo.

Mwezi Septemba Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), kupitia kwa Kaimu Katibu mkuu wake, Wilfred Kidao ilitangaza kuwa ratiba ya ligi haitapanguliwa tena mpaka imalizike mwezi Mei mwakani.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *