Chanzo cha Hasira za Samatta Jana

MSHAMBULIAJI nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ jana alionekana mwenye hasira kali mara baada ya timu yake kuambulia sare ya bao moja dhidi ya Lesotho kwenye mchezo wa kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON 2019).

Samatta ambaye ndiye aliifungia bao pekee Stars dakika 27 alionekana kurusha mikono na miguu hewani mara baada ya mwamuzi wa mchezo huo Abdillah Mahamoud Iltireh kutoka Somalia kupuliza filimbi ya mwisho kuashiria kumalizika kwa mchezo huo.

Akizungumza na waandishi wa habari waliohitaji kufahamu chanzo cha hasira zake mara baada ya mchezo huo kumalizika, Samatta alisema ni kutokana na matokeo huku akikiri yeye hapendi kushindwa.

“Hasira ni kutokana na tabia yangu ya kutokubali kushindwa, droo sio mbaya lakini tulikuwa nyumbani, tulihitaji ushindi kwa lazima ili kuweza kujiwekea mazingira mazuri ya kufuzu.

 

Mbwana Samatta
Mbwana Samatta

“Nadhani wachezaji wote walikuwa na hasira sio mimi peke yangu, labda tu kwavile mimi nilishindwa kujizuia ila hakuna aliyefurahia matokeo haya,”. Alisema Samatta.

Stars ina mtihani mgumu kufuzu fainali hizo kwani katika kundi L walilopo kuna timu nyingine za Uganda na Cape Verde ambazo zipo juu ya Stars kwenye viwango vya soka Afrika na duniani huku pia wakisifika kwa matumizi bora ya viwanja vyao vya nyumbani.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *