CHECHE: BADO TUNAKOMAA NA SAFU YETU YA USHAMBULIAJI

Kocha msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche amesema wanaendelea kuifanyia marekebisho safu yao ya ushambuliaji ambayo bado imeonyesha mapungufu katika kufumania nyavu.

Azam imekuwa ikipata ushindi mwembamba katika michezo yao mingi msimu huu kitu ambacho benchi la ufundi linazidi kufanya marekebisho.

Cheche ameiambia Simba Makini muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Mbao FC walioshinda mabao 2-1 kuwa moja ya idara ambayo wameiwekea mkazo ni ushambuliaji.

“Unajua washambuliaji wetu ni vijana wadogo ambao wanahitaji kupewa muda ili kuonyesha uwezo walionao na tunatarajia kuanzia msimu ujao watakuwa vizuri,” alisema Cheche.

Safu ya ushambuliaji ya Azam inaongozwa na Mbaraka Yusuph, Yahaya Zayd, Shaban Chilunda, Waziri Junior na Bernard Arthur ambao kasi yao ya ufungaji hairidhishi sana.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *