CHELSEA, PSG ZAPIGANA VIKUMBO KWA ENRIQUE

Baada ya kocha Antonio Conte wa Chelsea na Unai Emery wa PSG wakionekana kutaka kuonyeshwa mlango wa kutokea majira ya joto yajayo klabu hizo zinawania saini ya Meneja wa zamani wa Barcelona, Luis Enrique.

Enrique, 47, hana timu tangu alipoachana na Barcelona mwishoni mwa msimu uliopita ambapo anatarajiwa kuonekana tena uwanjani kuanzia msimu ujao.

PSG inamtazama Enrique kuchukua mikoba ya Unai ambaye alitolewa na Real Madrid kwenye michuano ya Ulaya hatua ya 16 bora huku pia wakimuwinda kocha Tottenham Hotspur, Mauricio Pochettino kama wakimkosa Mhispania huyo.

Chelsea ambao wiki ijayo watakutana na Barcelona katika mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi ya mabingwa ambao utaamua mustakabali wa Conte klabuni hapo.

Chelsea haina uhakika wa kumaliza nafasi nne za juu huku ikiwa pia haina uhakika wa kutwaa taji lolote msimu huu.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *