CHELSEA YAJITOA KWA SANDRO, UNITED SASA NJIA NYEUPE

Chelsea haiko tayari kutoa kitita cha pauni 60 milioni kwa ajili ya nyota raia wa Brazil, Alex Sandro wa Juventus ambapo Manchester United inapewa nafasi kubwa ya kumchukua mlinzi huyo.

Antonio Conte alikasirika baada ya kushindwa kumsajili Sandro majira ya joto yaliyopita na ameendelea kuwashauri mabosi wake kumnyakua mlinzi huyo mwezi huu.

Juventus ipo tayari kumruhusu Sandro kuondoka lakini inataka timu inayomuhitaji kutoa kitita cha pauni 60 milioni.

Chelsea wataangalia njia mbadala ya kutafuta beki wa bei rahisi huku ikiachia United njia nyeupe kwa ajili ya mlinzi huyo.

Meneja Jose Mourinho anataka kusajili walinzi wawili wa pembeni na kiungo mbunifu pamoja na mshambuliji katika vipindi viwili vya usajili ili kuimarisha kikosi chake.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *