Chenga za Kapombe Azam Hadi Kuibukia Msimbazi

HAKUNA kipindi kina presha kwa viongozi na mashabiki kama hiki cha usajili. Licha ya kwamba dirisha la usajili halijafunguliwa rasmi, tayari timu za ligi kuu zimeanza vita ya kuwania saini za nyota mbalimbali hasa ambao wamemaliza mikataba na timu zao.

Simba ilianza mapema mipango ya kumtwaa beki wa kulia wa Azam FC Shomari Kapombe na wakati dalili zikionekana kuwa nzuri kwao, Wanalambalamba waliibuka usiku wa jana na kufanya jaribio la kumuongezea mkataba beki huyo mara baada ya kutoka kwenye kambi ya Taifa Stars.

Ikionekana kama vile Kapombe alikuwa tayari kusalia Azam, vigogo wa Msimbazi waliharibu mpango huo kwa kumtangazia dau nono zaidi jambo ambalo lilimfanya mlinzi huyo aliyeibukia kwenye kitu cha Moro Kids mjini Morogoro kusitisha mpango wa kusaini usiku wa jana.

Shomari Kapombe alipokuwa akiichezea Simba miaka ya nyuma
Shomari Kapombe alipokuwa akiichezea Simba miaka ya nyuma

Vita ya kukamata saini ya beki huyo mwenye uwezo mkubwa wa kupandisha mashambulizi na hata kufunga mabao iliendelea tena leo ambapo majira ya jioni viongozi wa Azam walionekana wakiwa naye ofisini kwao Mzizima kabla hajaondoka na baadaye taarifa kutoka kuwa ameshasaini Msimbazi.

Mtandao huu umejaribu kuwatafuta viongozi wa Simba na Kapombe mwenyewe ili waweze kuelezea ukweli wa jambo hili lakini hakuna ambaye alipokea simu ingawa watu wao wa karibu wamekiri kuwa usajili huo umekamilika.

Tafadhali endelea kutembelea simbamakini.co.tz kwa taarifa mpya za usajili na nyingi za kimichezo

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *