CHILUNDA AMKARIBISHA PLUIJM VIZURI ATUPIA MANNE MWENYEWE

Mshambuliaji Shaban Idd Chilunda amefunga mabao manne na kuisaidia Azam kuibuka na ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda na kuingia nusu fainali ya michuano ya kombe la Kagame.

Chilunda amesaini mkataba wa miaka miwili na klabu ya CD Tenerife inayoshiriki ligi daraja la pili nchini Hispania juzi Ijumaa.

Chilunda alifunga mabao matatu ‘hat trick )’ ndani ya dakika 40 katika dakika za 18, 33 na 39 akiwa mchezaji wa kwanza kwa kufanya hivyo kwenye michuano hiyo.

Mchezo huo ni wa kwanza kwa kocha Hans van Pluijm kuiongoza Azam tangu alipochukua mikoba ya Mromania Aristica Cioba.

Mlinzi Rwatubiyaye Abdul aliifungia Rayon bao la kwanza dakika ya 42 baada ya mlinda mlango Razak Abalora kushindwa kuudaka mpira wa krosi.

Chilunda aliifungia tena Azam bao la nne kwa dakika ya 64 baada ya kuwazidi ujanja walinzi wa Rayon.

Manishimwe Djabel aliifungia Rayon bao la pili dakika ya 81 baada ya kupokea pasi akiwa ndani ya 18 na kupiga shuti la chini chini lililomshinda Abalora.

Mshambuliaji huyo amefikisha mabao saba akiwa kinara wa ufungaji akiwaacha kwa mbali Adam Salamba wa Simba, Jacques Tuyisenge wa Gor Mahia na Pierre Kwizera wa Rayon wenye mabao matatu kila mmoja.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *