CHILUNDA ASEMA SOKA LAKE LINAZIDI KUIMARIKA

Mfungaji wa bao pekee lililoipeleka Azam FC fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi, Shaban Idd ‘Chilunda’ amesema kadiri siku zinavyokwenda ndio anazidi kuimarika kwenye soka.

Chilunda ambaye amerejea kutoka majeruhi yaliyomuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu ameushukuru uongozi wa klabu hiyo kwa kumjali kipindi alichokuwa majeruhi.

Mshambuliji huyo alitokea benchi kwenye mchezo wa jana wa nusu fainali dhidi ya Singida United alitumia dakika mbili kufunga bao hilo na kuwapeleka Azam fainali.

Chilunda ambaye ametokea katika Academy ya klabu hiyo ameuambia mtandao huu kuwa kiwango chake kimezidi kuimarika na ataendelea kujituma ili kufanya vizuri zaidi.

“Mwenyewe najiona kuwa nazidi kuimarika hasa ukizingatia nimetoka kwenye majeraha lakini namshukuru Mungu kwa hapa nilipofikia,” alisema Chilunda.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *