CHIRWA APITA ANGA ZA OKWI, ANG’ARA MWEZI OKTOBA

Mshambuliaji wa timu ya Yanga, Obrey Chirwa amewapiku wachezaji Erasto Nyoni na Ibrahimu Ajib na kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Oktoba wa ligi kuu ya Vodacom.

Emmanuel Okwi wa Simba alikuwa wa kwanza kutwaa tuzo hiyo mwezi Agosti na kufuatiwa na beki wa kushoto Singida United Shafiq Butambuze mwezi Septemba ambapo raia huyo wa Zambia anakuwa mchezaji wa tatu kutwaa tuzo hiyo.

Chirwa aliisadia Yanga kupata pointi saba katika michezo mitatu ya mwezi huo iliyocheza na kupanda katika msimamo wa ligi kutoka nafasi ya sita iliyokuwepo mwezi Septemba hadi ya pili mwishoni mwa Oktoba.

Nyota huyo alifunga katika michezo yote mitatu ya Yanga mwezi Oktoba ambayo ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar mabao 2-1 (Kaitaba), Stand United walioshinda mabao 4-0 (Kambarage) na Simba sare ya 1-1 (Uhuru).

Chirwa atapokea kitita cha sh milioni moja kutoka kwa Kampuni ya Vodacom ambao ndio wadhamini wakuu wa ligi hiyo kama zawadi ya kushinda tuzo hiyo.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *