CIOBA AIBADILISHIA SINGIDA GIA ANGANI, AZAM YATINGA FAINALI

Mabadiliko ya kipindi cha pili yaliyofanywa na kocha mkuu wa Azam FC, Aristica Cioba yameisaidia kutinga fainali ya michuano ya kombe la Mapinduzi baada ya kuifunga Singida United bao moja katika mchezo wa nusu fainali ya pili.

Raia huyo wa Romania aliwaingiza kwa pamoja Bryson Raphael na Shaban Idd kuchukua nafasi za Yahaya Zayd na Joseph Mahundi ambao walibadilisha matokeo ya mchezo huo.

Shaban ndiye alifunga bao hilo dakika ya 78 muda mfupi baada ya kuingia na kuwaweka Azam kwenye mazingira ya kutetea taji hilo.

Singida walitawala sehemu kubwa ya mchezo huo ambapo walifanya mashambulizi mengi langoni mwa Azam lakini safu yake ya ushambuliaji ilikosa ubunifu.

Azam watacheza mchezo wa fainali dhidi ya URA Januari 13 katika uwanja huo huo wa Amani.

Azam ndio mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya mwaka jana kutwaa taji hilo kwa kuwafunga Simba bao moja kwenye mchezo wa fainali.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *