CONTE: Bado Sana, Tunataka FA pia

LONDON, Uingereza
KOCHA wa Chelsea Antonio Conte amesema anahitaji kutwaa kombe la FA ili kumaliza msimu kipekee kufuatia kufanikiwa kuchukua ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza usiku wa kuamkia leo.

The Blues wamekuwa mabingwa kwa mara ya tano huku wakisaliwa na michezo miwili kabla ya kumalizika kwa ligi, shukrani kwa bao la ‘jioni’ lililofungwa na Michy Batshuayi ugenini dhidi ya West Brom.

Vijana wa Conte watakutana na Arsenal katika fainali ya kombe la FA itakayofanyika Mei 27 kwenye uwanja wa Wembley.

chelsea-win-premier-league-afp_806x605_51494644373

“Kwangu kushinda taji katika msimu wa kwanza nchini Uingereza ni mafanikio makubwa, najivunia sana mafanikio haya,” Conte aliiambia BBC Sport.

“Wachezaji wangu wamenionyesha weledi mkubwa na kucheza kwa moyo kuhakikisha tunashinda taji hili.

“Tuna michezo miwili ya kusherehekea ubingwa wetu, na baadae tuufanye msimu huu kuwa wa kipekee kwa kutwaa taji la FA.” Alisema Conte.

Conte ambaye alianza kukinoa kikosi cha mabingwa hao baada ya kumalizika michuano ya Euro 2016 alisema kutumia mabeki watatu kulipelekea kipigo cha mabao 3-0 kutoka kwa Arsenal mwezi Septemba mwaka jana na kuanza kuona msimu mgumu kwao.

403F0DFA00000578-4501178-image-a-10_1494623423103

“Ilikuwa hali tete kwangu kwani baada ya mchezo dhidi ya Arsenal kumalizika nilikuwa sioni kitu chochote mbele katika kazi yangu na mawazo yangu katika soka,” alisema Conte.

“Lakini kwa sasa nimepata nguvu ya kubadilika na kufanya majukumu ya kubadili mfumo wa kiuchezaji uliopelekea leo kutwaa ubingwa.

“Wakati nafika hapa kulikuwa na msimu mbaya baada timu kumaliza nafasi ya 10 iliyoonyesha kulikuwa na matatizo makubwa.”

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *