COURTOIS AMHOFIA KANE KOMBE LA DUNIA

Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Thibaut Courtois anaamini nahodha wa Uingereza, Harry Kane ndiye tishio kubwa kwao watakapo kutana katika fainali za kombe la duniani nchini Urusi.

Courtois na timu yake ya Ubelgiji wapo kundi G na watakutana na Uingereza Juni 28 katika mchezo wa mwisho wa kundi hilo.

Kane amefunga 30 katika ligi kuu Uingereza msimu uliopita kwa timu yake ya Tottenham Hotspur na ndiye mshambuliaji pekee ambaye Courtois anamhofia.

“Uingereza ina wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu lazima tuwe makini na baadhi ya nyota wao.

“Lakini Kane ambaye anafunga mabao 30 kila mwaka yeye ni hatari zaidi na tunapaswa kumchunga sana,” alisema Courtois.

Ubelgiji itacheza na Misri leo katika mechi ya kirafiki lakini Mafarao hao watakosa huduma ya mshambuliaji Mohamed Salah ambaye ni majeruhi.

It's only fair to share...Share on Facebook
Facebook
Share on Google+
Google+
Tweet about this on Twitter
Twitter
Share on LinkedIn
Linkedin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *