COUTINHO AIKATA MAINI BARCELONA, ASEMA ANA FURAHA LIVERPOOL

Kiungo Philippe Coutinho amesema ana furaha katika klabu yake ya Liverpool baada ya taarifa kudai atajiunga na Barcelona katika dirisha la usajili mwezi Januari.

Miamba hiyo ya Catalunya ilijaribu kumsajili Coutinho majira ya joto yaliyopita lakini baada ya kushindwa kumpata mabingwa hao wamejipanga kurejea tena mwezi Januari.

“Ninacheza katika klabu kubwa duniani, nina furaha hapa. Kwa sasa mawazo yangu yapo kwenye timu yangu ya taifa lakini nina furaha na maisha yangu,” alisema Coutinho wakati akizungumzia mchezo wa kirafiki wa Brazil dhidi ya Uingereza utakaopigwa kesho.

Coutinho alikuwa nje ya uwanja tangu Oktoba 22 baada ya kuumia mguu lakini amesema amepona na yupo tayari kulitumikia taifa lake katika mchezo wa kesho kwenye uwanja wa Wembley.

“Nipo fiti asimilia mia, nilikuwa majeruhi na nililikosa mechi tatu lakini nimerejea na nipo tayari kwa mchezo wa kesho.

“Kuvaa jezi ya rangi ya njano ni heshima kubwa. Itakuwa heshima kwangu kama nitapata nafasi ya kucheza mechi hii, tunatarajia kucheza soka la kuvutia katika mchezo huu,” alisema Coutinho.

Coutinho anatarajia kukutana na mchezaji mwenzake wa Liverpool Dominic Solanke ambaye ameongezwa kikosini na Gareth Southgate kutoka timu ya vijana chini ya miaka 21.

It's only fair to share...Share on FacebookShare on Google+Tweet about this on TwitterShare on LinkedIn

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *